Exodus 29:24-26

24 aViweke vitu hivi vyote mikononi mwa Haruni na wanawe na uviinue mbele za Bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa. 25 bKisha vichukue vitu hivyo kutoka mikononi mwao, uviteketeze juu ya madhabahu pamoja na sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu nzuri ya kupendeza kwa Bwana, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto. 26 cBaada ya kuchukua kidari cha huyo kondoo dume wa kuwekwa wakfu kwa Haruni, kiinue mbele za Bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa, nayo itakuwa fungu lako.

Copyright information for SwhKC